MSANII mpya wa Bongo Fleva na memba wa Lebo ya King’s Music, Tommy Flavour ameeleza siri ya kudumu kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lynn’.
Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Tommy Flavour anasema kuwa, uhusiano wao umefanikiwa kutokana na utulivu wao tangu walipoanzana miezi saba iliyopita.
“Mimi na Official Lynn sasa hivi tuna muda wa miezi saba tangu tumekuwa pamoja, ishu ya kwanza ilikuwa ni utayari na usiriazi, hivyo ndivyo vitu vinavyofanya uhusiano wetu kuwa na nguvu,” anasema Tommy Flavour akikanusha kwamba uhusiano wao haukuwa ni kiki.
Hakimu wa Wilaya ya Nzega, Joseph Mwita, aliiambia mahakama hiyo kuwa mtumishi huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) (2) na 3 (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.
Awali, mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru aliiambia mahakama kuwa, kati ya Agosti 26 na Agosti 28, mwaka huu, kwa nyakati tofauti, mshitakiwa huyo, akiwa eneo la Merry Pub mjini Nzega, aliomba rushwa ya shilingi milioni 1,500,000/= kutoka kwa mfanyabishara huyo aliyetajwa kwa jina la Sahani Katuli.
Mtuhumiwa huyo alidaiwa kuomba rushwa ili asimchukulie hatua za kisheria kwa kutotoa risiti ya EFD katika nyumba yake ya kulala wageni ya Kipozo iliyoko mjini Nzega.
Mazengo aliendelea kuiambia mahakama kuwa, Agosti 29, mwaka huu, mshitakiwa alikamatwa na maofisa wa Takukuru Wilaya ya Nzega akipokea rushwa ya shilingi laki nne kati ya zile shilingi milioni 1.5 alizoomba kutoka kwa mlalamikaji Katuli baada ya kuwekewa mtego.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka kwa mara ya pili, mshitakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa.
STORI: KHADIJA BAKARI, DAR
