×

Museveni Asema Hajui Mwelekeo wa Wapinzani Tz – Video

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema si rahisi kwa mgombea urais kuibuka na ushindi katika nchi za Bara la Afrika bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa chenye mwelekeo mzuri.
Museveni amesema hayo leo Alhamisi, Novemba 5, 2020, wakati akizungumza katika hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kuimarisha usalama na kufungua masoko yao kwa ajili ya bidhaa za kilimo na viwandani za nchi wanachama na ka  Tanzania kununua sukari na mahindi kutoka Uganda.

“Kwa niaba ya Waganda natoa hongera kwa Rais Magufuli, natoa hongera kwa ushindi huo mlioupata kwa amani, vilevile niwapongeze miezi michache nyuma TZ ilitangazwa imeingia kwenye uchumi wa kati, mmetuwahi kidogo lakini na sisi tunakuja.

 

“Leo naona hapa Rais wa Zimbabwe, wawakilishi kutoka Msumbiji na maeneo mengine hii ni kwa sababu ya mshikamano wa Mwalimu Nyerere na viongozi wengine walioipigania Afrika, bila wao hawa wasingekuwepo hapa.

 

“Baada ya uhuru viongozi waligawanyika, wengi walichukua mstari wa kuwa vibaraka wa nje, wachache waliipigania Afrika akiwemo Mzee Nyerere, Kaunda, Nkrumah na wengine, hayati Mzee Moi alitukumbusha neno moja la nyayo akimaanisha alifuata nyayo kisiasa za Mzee Kenyatta.

 

“Uchaguzi 2015 niliweka TBC1 nikawa na hofu sana (kuhusu CCM) nikasema inakuwaje, baadaye nikaona mama mmoja (Mabula) ameongoza kwa kura nyingi Ilemela, mwaka huu.  Niliweka TBC nikaona Hai, majimbo ya mwanzo kabisa Hai, Newala, Mtwara,  nikasema basi.

 

“Kwa kawaida huwa sifuatilii mambo ya Watanzania ila wakati wa uchaguzi najikuta naweka TBC1 nione uchaguzi unaenda vipi nadhani ni kwa sababu najua mwelekeo wa CCM kisiasa, vyama vingine sijui mwelekeo wao.   Afrika ili kufaulu lazima tukumbuke hili la mwelekeo wa kisiasa,” amesema.

Leave a Comment