
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanafanya mazoezi na kuepuka ulaji usiofaa ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo Shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari ambayo yamekuwa chanzo Cha vifo na usumbufu kwa wananchi.
RC Kunenge amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa wiki ya kitaifa ya kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza iliyoanza November 07-14 kwenye Viwanja mnazi mmoja ambapo amesema Katika wiki hiyo wananchi watapata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali bure na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
Aidha RC Kunenge amesema kwakuwa magonjwa hayo yanaweza kuzuilika ni vyema wananchi wakaanza kuchukuwa tahadhari mapema kwa kuhakikisha wanazingatia ulaji Bora, kupunguza ulevi usiofaa,kupunguza uvutaji wa sigara na kuzingatia michezo.
Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Upande wa Serikali itaendelea kutoa elimu ya kutosha ya namna Bora ya kukabiliana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha na kuongeza miundombinu mbalimbali ya Afya.
Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali za kitabibu duniani, magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakichangia vifo vingi vya watu kutokana na jamii nyingi kutojua namna ya kujikinga au kukabiliana nayo.