×

JPM Amwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemwapisha Profesa Adelardus Kilangi, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, leo Jumatatu, Novemba 9, 2020, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

 

Kilangi anakuwa mteule wa kwanza wa Magufuli tangu aingie madarakani awamu hii pia anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili, baada ya kipindi cha kwanza kumalizika Novemba 5, 2020.

 

Akizungumza baada ya uapisho huo, Magufuli amesema: “Watanzania wanapenda kuona mafanikio mengi kupitia ofisi yako, wasingependa kuona kesi za serikali kila mara zinashindwa na wakati Mwanasheria Mkuu yupo, wangependa kuona kesi zinazohusu serikali na mali zao zinatetewa kwa haraka.

 

“Sisi tumekupa kwa niaba ya Watanzania, katika kipindi chako cha mwanzo ulifanya vizuri na sasa tumekupa tena ukafanye vizuri zaidi, ukamtangulize Mungu mbele, tunaamini utafanya mazuri, tunakupa pole lakini pia tunakupongeza,” amesema Magufuli.

 

Awali baada ya uapisho huo, Kilangi amesema: “Mheshimiwa rais ninapoanza kipindi cha pili katika majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ninaanza majukumu haya nikiwa na uelewa zaidi juu ya majukumu yangu, lakini kuhusu pia changamoto ambazo nitakabiliana nazo.

 

“Ninaahidi kufanya kazi kwa akili yangu yote kwa nguvu zangu zote, kwa uwezo wangu wote na nikishirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali katika kutatua changamoto hizo.”

 

Leave a Comment