WINGA wa Tanzania, Simon Msuva, ameripotiwa kujiunga na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwa mkataba wa miaka minne akitokea Difaa El Jadid ya nchini humo.
Wydad Casablanca walifika hatua ya nusu fainali klabu bingwa Afrika msimu huu na walishika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Morocco msimu ulioisha.
