×

Kingdom Leadership Network Tanzania na Chuo cha Regent cha Marekani Kutoa Kozi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kingdom Leadership Insititute, Dkt. Frederick Ringo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) walipokuwa wakitangaza muungano huo.

TAASISI ya Kingdom Leadership Network Tanzania na Chuo Kikuu Regent cha nchini Marekani wameungana na katika kutoa kozi mbalimbali hapa nchini ikiwemo kozi za Uongozi, Biashara, Ujasiriamali na nyinginezo.

Sehemu ya wadau waliohudhuria mkutano huo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi wa taasisi ya Kingdom Leadership Network, Isaac Mpatwa, ambayo inaendesha chuo cha Kingdom Leadership cha hapa nchini amesema wameungana na chuo hicho ili kutoa huduma za pamoja zijulikanazo kama Leadership Summit.

Mmoja wa wawezeshaji mpango huo, Jason Benedict kutoka nchini Marekani akizungumza na wanahabari kwenye mkutano huo.

Mpatwa amesema kituo hicho cha mafunzo ya pamoja kitaitwa Tanzania Business Development Centre ambapo lengo kuu la mpango huo ni kuwaandaa viongozi bora, wafanyabiashara na wajasiriamali.

Mpatwa amesema kozi hizo zinatarajiwa kuanza Jumamosi ijayo Novemba 14 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel jijini Dar.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kingdom Leadership, Isaac Mpatwa akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi huyo amesema mafunzo hayo yatatolewa na wakufunzi wa kimataifa wakiwemo viongozi waandamizi wa hapa nchini na kuwaomba viongozi wengine, wafanyabiashara, wajasiriamali kujitokeza kwenye mafunzo hayo.

Ameendelea kusema kuwa wahitimu wote wa mafunzo hayo watapata cheti kimoja na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Regent cha nchini Marekani walichoungana nacho katika kutoa mafunzo hayo.

Mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Katibu Mtendaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Godwill Wanga ambaye alimuwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Mpatwa amesema kwa maelezo zaidi ya kujiunga mafunzo hayo unaweza kuwasiliana nao kupitia [email protected] au www.kingdomleadership.ne.tz 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS GPL

Leave a Comment