The House of Social Media
gunners X

Tanzania Pekee Yatajwa Kutokuwa na Corona Ulimwenguni

0

RIPOTI iliyotolewa na Kituo cha Bara la Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti magonjwa (ECDC) na kisha ripoti hiyo kuchambuliwa na kusomwa na kituo kikubwa cha habari cha nchini Ujerumani cha Deutsche Welle (DW) imeitaja Tanzania kuwa nchi pekee duniani ambayo haijaripoti kisa chochote cha mgonjwa wa Corona kwa wiki nne (4) zilizopita huku ikiwa salama na ugonjwa huo hatari duniani kwa sasa kwa takribani wiki 46.

 

Ripoti hiyo iliyotolewa na kituo hicho chenye makao makuu yake jijini Solna nchini Sweden, inaeleza kwamba wakati dunia nzima ikiwa kwenye giza totoro na isijue cha kufanya kwa kuendelea kuripoti visa vya Corona kila kukicha, Tanzania iko salama kabisa na balaa hilo na watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku bila ya vizuizi wala masharti yoyote ya Corona.

 

Nani kama Mungu? Shukrani na pongezi ziende kwa Mungu kupitia kwa rais mwenye maono na mchamungu Dkt John Pombe Magufuli, aliyelivusha taifa hili kwa misimamo yake ya kumtegemea na kumshirikisha Mungu pekee katika jambo hili.

 

Wakati serikali zote duniani zikifunga nyumba za Mungu na ibada, Rais Magufuli yeye alisimama pekee yake duniani licha ya kupigwa vita na kulikabidhi jambo hili kwa Mungu. Leo Mungu ametenda miujiza kwa Tanzania. Hakuna Corona wala cha shangazi yake na Corona hapa Tanzania. Wengine wanakumbuka shuka leo wakati kumeshakucha. Mungu ametenda na kuishangaza dunia kupitia kwa Dkt John Pombe Magufuli. Mpaka sasa, Tanzania ndiyo nchi pekee haina Corona duniani.

Leave A Reply