×

Spoti Xtra Jumanne Lapokelewa kwa Kishindo – (Pichaz + Video)

KAMPUNI namba moja ya habari nchini, Global Publishers inayochapisha magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, kwa kutambua kiu ya wasomaji wao kupata habari makini za michezo na burudani, leo Jumanne, Novemba 17, 2020, imezindua gazeti lake jipya la michezo la Spoti Xtra Jumanne ambalo litakuwa linatoka kila Jumanne ya wiki.

Akizungumza na Global TV Online, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha Global Publishers, Anthony Adam, amesema Spoti Xtra Jumanne ni gazeti jipya lililosheheni habari mbalimbali za michezo na burudani za hapa nyumbani Tanzania na nje ya mipaka ya nchi, zilizoandikwa na kuhaririwa na waandishi mahiri kwa ajili ya kukidhi na kukata kiu ya wanamichezo wote nchini.

“Kama mnavyojua Global Publishers hapo kabla haikuwa na gazeti la michezo lililokuwa likitoka siku ya Jumanne hivyo kuwaachia wasomaji wetu kiu kubwa ya taarifa za kimichezo, hali hiyo iliusukuma uongozi wetu kuja na Spoti Xtra Jumanne ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu.

“Kwa muda sasa tumekuwa mtaani kutangaza ujio mkubwa wa Gazeti la Spoti Xtra Jumanne, hatimaye leo tumefanikiwa na gazeti hilo tumeliingiza sokoni, kwa Tsh 500 tu unajipatia nakala ya Spoti Xtra Jumanne. Tunashukuru wasomaji wetu wamelipokea kwa kishindo, mapokezi ni chanya.

“Na sisi timu ya masoko tumeingia mtaani kukutana na wasomaji mbalimbali ambao wameonyesha kufurahishwa sana na ujio wa gazeti hili kwani litaondoa kiu yao ya habari za michezo kwa siku ya Jumanne, tutaendelea kuboresha zaidi na zaidi ili kuwapa wanachokitaka,” alisema Adam.

Aidha, Adam amewaomba wasomaji kuendelea kuiamini Kampuni ya Global Publishers na bidhaa zake kwani imekuwa ikisikiliza zaidi mapendekezo yao na kuwaletea bidhaa wanazohitaji lakini kampuni hii imekua ikienda mbali zaidi na kufanya promosheni mbalimbali kurudisha fadhira kwa wasomaji wake.

 

Leave a Comment