
STAA Bongo Fleva, Aslay Isihaka, hana tambo, mbwembwe wala makelele mengi, lakini anakimbiza mwizi kimyakimya na kuweka rekodi zake za kibabe Bongo. Taarifa ikufi kie kuwa, Aslay ametwaa tuzo nne kwa mpigo kutoka kwenye mtandao wa kusambaza muziki ya Boomplay Music.
Aslay amekabidhiwa tuzo hizo kufuatia EP (Extended Playlist) yake ya Kipenda Roho kufi kisha zaidi ya wasikilizaji milioni moja ndani ya mtandao huo. Nyimbo zake mbili za Likizo na Natamba, nazo zimeweka rekodi zake baada ya kufi kisha wasikilizaji zaidi ya laki tano.
Kwa hatua kubwa alizopiga Aslay kwa kutwaa tuzo hizo nne kwa mpigo, kwa ameungana na wasanii wengine kama Faustina Charles ‘Nandy’, Juma Mussa ‘Jux’ na Yusuf Mbwana ‘Mbosso’ ambao nao wametwaa tuzo hizo japokuwa yeye anawazidi kwa idadi ndani ya mwaka huu.
Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilizungumza na meneja wa Aslay, Shaban Chambuso ambapo alifunguka kuwa, wamefurahishwa mno kuona msanii wao ameweza kuonekana kwenye tuzo hizo na kwamba siyo jambo dogo hivyo wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.
“Kwanza kabisa tunamtanguliza Mungu kwa kila jambo. Pia tunashukuru sana kwa hiki tulichoweza kupata kwani siyo kitu kidogo msanii kupata tuzo nne kwa mpigo, ni jambo kubwa sana na la heshima. “Hapa ndipo tunaona kuwa Aslay amekua kimuziki kwa kiasi gani,” anasema Chambuso.
Aslay ni mmoja wa wasanii wanne waliokuwa wakiunda Yamoto Band ambapo baada ya kusambaratika kwake, kila mmoja alianza kujitafutia malisho kivyake.
STORI: KHADIJA BAKARI, DAR