
MSANII wa Bongo Fleva, Enock Rashid ‘Enock Bella’, amefungu kuwa kipindi lilipovunjika kundi la Yamoto Bendi alikata tamaa kiasi cha kutaka kuacha muziki.
Enock ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Chukua’ ameliambia Amani kuwa alipoteza muelekeo kabisa hadi kufi kia hatua ya kutaka kwenda kwa mkubwa Fella kuomba kufanya kazi Wasafi.
“Nilikata tamaa sana kiasi kwamba nilitaka kuacha muziki kabisa. Unajua nilipoteza muelekeo kabisa, hadi nikataka kwenda kwa Mkubwa Fella kuomba kufanya kazi Wasafi.
“Lakini sasa hivi namshukuru Mungu nimeweza kufuta fi kra potofu na ninafanya kazi zangu mwenyewe na mashabiki wameshauelewa muziki wangu,” alisema Enock.
STORI: Khadija Bakari