BARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi uliofanyika na 8 Oktoba 7 na 8, 2020.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde Jumamosi tarehe 21 Novemba 21, 2020, yanaonyesha kati ya shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 40, Dod’s Bridge ya jijini Mbeya inaongoza kundi hilo huku Mkoa wa Kagera ukiingiza shule mbili.
Amebainisha shule kumi ambazo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, zimeongeza ufaulu ambapo Mwandu-Kisesa ya Mkoa wa Simiyu imeongoza kundi hilo.
Pia amezitaja shule kumi ambazo kwa miaka mitatu mfululizo, zimeshuka ufaulu kwa kiasi kikubwa zikiongozwa na Chororo ambapo ya mwisho ni Ng’ongolo zote za Mtwara.

