×

EFG Inavyotengeneza Wanawake Wenye Nguvu ya Kiuchumi – Video

 

Equality for Growth (EfG) ni taasisi ya kitaifa yenye maono ya kutengeneza wanawake wenye nguvu kiuchumi katika sekta isiyo rasmi. Taasisi imejengwa katika muundo utakaoweza kuwawezesha wanawake wa sekta isiyo rasmi kuwa na sauti ya pamoja na kuweza kusimamia haki zao za kisheria na haki za binadamu kwa ujumla na kukuza utetezi na ujengaji wa uwezo katika kutokomeza umaskini.

 

Walengwa wanaonufaika na kazi za shirika la EfG ni wanawake waliojiajiri katika sekta rasmi na isiyo rasmi hasa wanawake wafanyabiashara katika masoko. Mpaka sasa shirika linafanya kazi katika mikoa 9 ya Tanzania Bara ikiwemo Mbeya, Mwanza, Iringa, Shinyanga, Lindi, Mtwara, Mara, Lushoto-Tanga na Dar es salaam katika masoko 15 ya Manispaa ya Ilala na Temeke.

 

Katika kipindi cha janga la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, Shirika lilitembelea na kufanya mahojiano mafupi na wanawake wafanyabiashara sokoni ili kuweza kufahamu changamoto za kijamii, kibiashara na kiuchumi walizokutana nazo kama wafanyabiashara, walezi na tegemezi wa familia zao.

 

Kwa kipindi hiki baada ya kuisha kwa maambukizi ya COVID-19, Shirika pia tumefanikiwa kurudi kwa wanawake hawa ili kuweza kujua namna walivyokabiliana na changamoto walizokutana nazo kipindi cha COVID-19, lakini pia kufahamu ni njia zipi walizozitumia ili kujikwamua kiuchumi na kuhakikisha biashara zao zinaendelea kustawi.

 

Simulizi hizi za wanawake sokoni zina lengo la kuwahamasisha wanawake wengine juu ya njia mbadala za ufanyaji biashara lakini pia kuiomba serikali kufanyia kazi changamoto zingine wanazokutana nazo katika biashara zao za kila siku hasa katika sekta isiyo rasmi.
INSTAGRAM: @equalityforgrowth
FACEBOOK: @equalityforgrowth
TWITTER: @EfGtz
YOUTUBE: Equalityforgrowth EFG

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment