
KITENDO cha msanii Koffi Olomide kwenda kula kwenye mgahawa wa msanii Shilole, hakikuishia kwenye kula tu bali na kuzungumzia kazi.
Hayo ameyaeleza Shilole alipokuwa akiitambulisha kwa waandishi wa habari lebo ya ShishiGang na msanii wa kwanza kumsaini.
Pamoja na mambo mengine, Shilole alielezea matunda ya kutembelewa na msanii huyo kwenye mgahawa wake siku mbili zilizopita.
“Nashukuru ujio wa Koffi haUkuniacha hivihivi, kwani tumezungumza mengi ikiwemo kwenda kutengeneza naye kolabo nchini Ufaransa. Amenipa mwaliko maalum na amesema tutarekodia kwenye studio yake na nitafikia kwenye hoteli yake ya nyota tano anayoimiliki nchini humo,” amesema Shishi.
Msanii huyo ambaye awali katika ukurasa wake aliandika kumshukuru Diamond Platnumz kumpelekea msanii huyo na kueleza siyo mara ya kwanza kumpelekea wasanii. Aliwataja wasanii wengine ambao amewahi kumpelekea kuwa ni pamoja na #Wizkid na #TiwaSavage.