×

Mtango Alivyomchapa Mfilipino Aliyekuwa Akiumezea Mate Mkanda Wake

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni kama ‘zari’ kwa Wabongo pale Bondia Mtanzania, Salim Mtango alipomchakaza  bondia wa kimataifa kutoka Ufilipino, Eduardo Mancito, muda mfupi kabla ya Bondia Iddi Pialali kumchapa  Bondia wa Kimataifa, Arnel Tinampay naye kutoka Ufilipino katika pambano la raundi nane.

Mtango na Mancito ndiyo walioanza kucheza pambano la utangulizi akitetea mkanda wake wa UBO uliokuwa ukiwaniwa na Mfilipino huyo.

Mtango (kulia) na Mancito wakikiwasha.

Hata hivyo baada ya kuupata mkanda huo, Mfilipino huyo aliambulia kipigo na mkanda huo kuendelea kubaki hapa nchini ukishikiliwa na Mtango.

Mfilipino Mancito akibebeshwa konde.   
Mancito akivuja damu juu ya baada ya kuchanwa na sumbwi.

Mtango akimpelekea Mancito konde la uso. 

Mwamuzi wa pambano hilo, Anthon Ruta akimuinua juu mkono Mtango akiashiria kuimtangaza ubingwa wa mkanda huo wa UBO.     HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL    

Leave a Comment