×

Ndugai: Tutaendelea Kuwatambua Wabunge Walioapishwa

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema, Bunge litaendelea kuwatambua wabunge wote walioapishwa wakiwemo 20 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 19 wa Viti Maalum na mmoja aliyeshinda katika uchaguzi mkuu.

 

Ameyasema haya leo Novemba 30 wakati akaiwaapisha wabunge wawili, Humphrey Polepole na Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.

“Nashangaa wanawasonga hawa 19, huyo mmoja wamemgwaya? Wakiweza wamfukuze lakini sisi tumeshamwapisha na tunamtambua hayo yanayoendelea huko ya kwao,” amesisitiza.

Aidha amesema hivi karibuni atawapanga wabunge katika kamati mbalimbali baada ya rais kuunda baraza la mawaziri.

“Kufikiri kwamba Bunge ni ukumbi wa Bunge peke yake ni fikra finyu sana, kwa hiyo wabunge wote wa Bunge la 12 tuliowaapisha tunaendelea kuwatambua ni wabunge kamili ikiwa ni pamoja na wale 20 wa  CHADEMA, kumi na tisa na yule mmoja aliyechaguliwa ambaye ni Mheshimiwa Aida Khenan,” alisema.

 

Leave a Comment