×

Serikali Yafafanua Hoja, Ajira za Waalimu

KATIBU  Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga; Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro;  na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, jana Novemba 30, 2020, wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu.

 

Ufafanuzi huo umetolewa leo katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI –  jijini Dodoma   baada  kutokea hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari  kuhusu ajira  mpya za walimu zilizotangazwa hivi karibuni.

 

 

Nyamhanga  amesema hoja kubwa ilyojitokeza ni kwa jina la  mwalimu mmoja kujitokeza katika kila ukurasa na kuonekana mara 196, badala ya mstari wa  maelezo ya Jedwali (sub- titles) lakini shule aliyopangiwa ni moja, pamoja na jina hilo kujirudia  halikuchukua nafasi   ya mwombaji  yoyote  ya walimu waliotakiwa kuajiriwa au kuathiri  idadi ya waalimu  waliotakiwa kuajiriwa na  tayari marekebisho yamefanyika.

 

Amefafanua pia kuwa shule binafsi kupangiwa mwalimu, serikali imekuwa ikiingia ubia na baadhi ya shule binafsi ambazo hupokea  wanafunzi wenye uhitaji maalum, shule hizo hupangiwa  walimu na  kupewa ruzuku ya uendeshaji, hivyo Shule ya Mwalimu Tutuba ilikuwa katika mchakato wa kuingia  ubia na serikali lakini haukukamilika, hivyo serikali baada ya  kujiridhisha mwalimu aliyepangiwa katika shule hiyo amepangiwa  katika shule ya sekondari Malagarasi.

 

Kwa upande wa  wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017, 2018 na 2019 kupangiwa vituo vya kazi, ameeleza  waombaji wa ajira walitumia  mwaka wa kuhitimu chuo badala  ya mwaka wa kuhitimu  kidato cha nne ambapo waombaji 27 waliandika mwaka 2019, waombaji 27 waliandika mwaka 2019 na waombaji 13 waliandika mwaka 2017, hivyo serikali ilihakiki vyeti vyao  na kubaini  kuwa waombaji hao walihitimu  kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

 

Aidha amewalekeza  wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kuhakiki vyeti halisi  vya waliopata ajira na kujiridhisha  kabla ya kutoa barua  za ajira, na kusisitiza kuwa endapo  itabainika  kuwepo udanganyifu au kasoro za vyeti vya kitaaluma  wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

&nbsp

Leave a Comment