×

Arteta: Spurs Wapo Vizuri Zaidi Yetu

BOSI wa Arsenal, Mikel Arteta, amekiri kuwa Tottenham inastahili kuwa juu kwenye msimamo wa Premier kutokana
na kufanya vizuri, Leo Jumapili, Arsenal na Tottenham zitavaana kwenye Uwanja wa Tottenham katika mechi ya Premier.

 

Kuelekea mchezo huo, Arteta amekuwa kwenye presha kubwa kutokana na hali ya timu yake ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo. Tottenham ni ya kwanza kabla ya mechi za jana.

 

Kocha huyo amesisitiza kuwa msimamo haudanganyi na Tottenham inayonolewa na Kocha Jose Mourinho walitumia
vyema dirisha la usajili na kuwa bora.

“Msimamo uko vile kwa sababu wanastahili kuwa pale kuliko sisi, ni kweli safari hii wamefanya vizuri kuliko Arsenal “Hilo tukubali, lakini kuelekea mchezo wetu bila kujali tunakutana na timu ya aina gani, malengo ni kuondoka na ushindi.

“Ninaamini tutaenda kushinda, wachezaji wangu wanajiamini na wanajua umuhimu wa mchezo huo,” alisema Arteta.
Kwa upande wa Mourinho, alisema kuwa: “Kwa sasa tupo kwenye nafasi nzuri, hivyo bado tunahitaji kuendelea kuwa hapo kwa kupata pointi za Arsenal, kuwafunga wao litakuwa ni jambo zuri na zawadi kwa mashabiki wetu.

 

“Unapocheza na Arsenal ili kushinda unatakiwa kufanya vizuri, ukiangalia msimu huu tupo nafasi nzuri na tunataka kuendelea kuwa hapo.”

Leave a Comment