×

GSM Kuwapeleka Mtu na Mpenzi Wake Hifadhi ya Ngorongoro Kutalii

KAMPUNI ya GSM imetangaza habari njema kwa wateja wote watakaotembelea na kufanya manunuzi kwenye maduka yao yaliyopo Mlimani City Dar, Nyerere Road, Msasani Mall na Duka lao lililopo Dodoma ambalo linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Akizungumza na Wanahabari kwenye duka lao lililopo Mlimani City Dar, Afisa Biashara Mkuu wa GSM Group of Companies, Allain Kichonjo amesema promosheni ambayo imeshaanza desemba hii nitakwenda mpaka mwishoni mwa januari mwakani.

Afisa Biashara Mkuu wa GSM Group of Companies, Allain Kichonjo alipokuwa akitangaza promosheni hiyo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Smart Deus na kulia ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Fatma Farah. 

Kichonjo amesema wateja wote watakaotembelea maduka hayo na kufanya manunuzi watapata nafasi ya kuingia kwenye droo ambayo itawawezesha kujishindia zawadi ya pesa taslimu, kupambiwa nyumba kisasa kabisa kwa kutumia fenicha zao, kujishindia safari ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na zawadi nyinginezo.

Sehemu ya seti ya masofa ikiwa dukani Mlimani City.

Kichonjo amesema mteja atakayejishindia safari ya kwenda kutalii hifadhi ya Ngorongoro atapata ofa ya kwenda na mpenzi wake na kugharamiwa kila kitu na kampuni hiyo akiwa kwenye safari hiyo.

Maduka ya GSM yamejizolea umaarufu kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo fenicha, vyombo vya ndani, mavazi na nyinginezo.

Muonekano wa moja ya vitanda dukani hapo.

Kichonjo amesema pamoja na zawadi hizo pia wateja hao wanaweza kujishindia zawadi ya kitanda cha kisasa kabisa.           HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment