×

Kilichomuua James Bond Chabainika

BAADA ya kupita mwezi mmoja na kidogo tangu nguli wa filamu nchini Marekani Sean Connery ‘James Bond’
afariki dunia, hatimaye taarifa zilizosababisha kifo chake zimevuja na kwamba mwamba huyo aliondoka kwa  ugonjwa wa Nimonia na magonjwa ya uzee.

 

Bond alifariki dunia Oktoba 31, mwaka huu akiwa usingizini, huku familia yake ikidai kuwa mzee wao huyo alifariki kwa mapenzi ya Mungu na kwamba hata umri wake wa miaka 90 ulikuwa kielelezo tosha kuwa alistahili kurejea kwa
Mungu wake.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ambao wanadai kuwa wamefanikiwa kupata cheti cha kifo cha nguli huyo, wameeleza kuwa Bond alifariki kwa ugonjwa wa Nimonia ambao ulisababishakufeli kwa mfumo wa upumuaji na moyo kushindwa kufanya kazi pia magonjwa ya uzee yalichangia.

Leave a Comment