×

Harmonize Ampiga Biti Kondeboy wa Simba

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya Konde Gang, Harmonize, wikiendi alijikuta katika hali ya tafrani baada ya kukataza watu kutumia jina la #Kondeboy kwa mchezaji wa Simba SC, Luis Miquissone,  akidai linatumika kimakosa kwani ni jina lake na angeombwa kulitumia.

 

Harmo amekomenti kwenye moja ya ujumbe uliokuwa umepostiwa kwenye mitandao ya kijamii ukihoji  kiwango cha ubora wa soka alichokionyesha Luis Miquissone, raia wa Msumbiji, baada ya game na Plateau ya Nigeria.

 

“Baba hilo jina is a brand usiligawe bila makubaliano, ana mtoto anaitwa Zurekha, umeongea naye mmekubaliana kuuza jina la baba yake?” aliandika Harmonize.

Leave a Comment