×

Wawili Mbaroni Kwa Tuhuma za Wizi Zaidi ya Mil. 100

WATU wawili wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma kuibia kampuni ya Diamond Motors kiasi cha zaidi ya Shilingi  Mil. (100) 176,263,573.89.

 

Watuhumiwa hao ni Emmanuel Sabuni na Linda Mtengule ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wamesomewa mashtaka yao na  Wakili wa Serikali, Yusuph Abood mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

 

Katika shtaka la kwanza linalowakabili watuhumiwa hao ni pamoja na wizi wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi  176,2635,73.89. Shtaka la pili ni la kugushi nyaraka ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa hao kati ya tarehe Januari Mosi 2019, na Desemba 31, 2019, walighushi mihuri ya  kampuni ya Mac Auto Accessories kwa lengo la kujipatia fedha.

 

Shitaka la tatu ni kughushi nyaraka ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2019, na 31 Desemba 2019 walighushi mihuri ya kampuni ya Degraglo Services Agency Ltd kwa lengo la kujipatia fedha.

Shtaka la mwisho ni washtakiwa hao wanadaiwa kughushi nyaraka za kampuni ya Brand Tyres kwa lengo la kujipatia fedha.

 

Baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, washtakiwa walikana mashataka yao. Hakimu Kabate aliwapa masharti ya dhamana kwa kutoa shilingi mil. 88  kudhaminiwa na mdhamini mmoja kwa kila mshtakiwa pamoja na kusaini bondi ya shilingi mil. 10.

 

Washtakiwa hao wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana na shauri hilo litatajwa tena Desemba 23, 2020.

Leave a Comment