×

DAS Ashauri Wanawake Nao Walipe Mahari

KATIBU  Tawala wa wilaya ya Bukoba (DAS), mkoani Kagera, Kadole Kilugala, amesema kuwa kama suala la mahari ni lazima katika jamii yetu basi itolewe kwa pande zote mbili, yaani mwanamke apeleke zawadi upande wa mume na mume afanye vivyohivyo ili kuweka usawa wa kijinsia.

 

Amesema kuwa suala la mahari la upande mmoja ndiyo linaonekana kuwa  linachochea masuala ya ukatili kwani wanaume huamua kuwafanyia chochote wanawake waliowaoa kwa kigezo cha wao kutoa mahari.

 

“Kama mahari ni lazima katika jamii yetu basi sote tuweze kutoa na kila mtu atoe kila alichonacho, mwanamke apeleke zawadi kwa mwanaume na mwanaume apeleke zawadi kwa mwanamke, tungeweza kutengeneza usawa kwa sababu mahari inatufanya tukose usawa wa kijinsia,” amesema.

 

Leave a Comment