
Hili ni soko la kisasa maarufu kama Soko la Chuno linalojengwa ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, soko hili ni matokeo ya usimamizi mzuri wa fedha uliofanywa na serikali ya awamu ya tano katika fedha zilizotolewa kwa mkopo toka Benki ya Dunia.

Awali fedha hizo zililenga ujenzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo dampo la kisasa na barabara za ndani, baada ya kuridhishwa na usimamizi huo, Benki hiyo iliamua kuongeza Bilioni 21.6 ambapo Bilioni 4.8 zilielekezwa katika ujenzi wa soko hili.

Soko hilo litakuwa na vizimba 193 vya biashara, bucha nane, vyumba vinne vya ofisi, sehemu Nne za kuuzia vyakula, Vyoo vinne, stoo saba, sehemu kwa ajili ya mashine za kutolea fedha (ATM) na sehemu ya matangazo.

Vilevile kutakuwa na sehemu saba za kushushia mizigo na sehemu mbili za maduka ya jumla pia eneo la maegesha ambalo litakuwa na uwezo wa kuegesha magari 81 kwa wakati mmoja.