
Kinga ya COVID-19 ipo mbioni kuanza kutolewa nchini Marekani, lakini kuna wengi wameonekana kutia mgomo.
Rapa Offset ametangaza kuikataa chanjo hiyo kwa sababu aliyoitaja kwamba haiamini, alipokutana na TMZ wikendi iliyopita alisema; “Siiamini hata hivyo, sitaki kuwa sehemu ya majaribio.” alisema Offset.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa New York Times, chanjo hiyo itaanza kujaribiwa na watumishi wa ikulu ya Marekani.
Rais wa Mareakani Donald Trump amebadili mpangowa kuwapa chanjo ya corona maafisa wa White House katika siku chache zijazo.
Awali maafisa walisema maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupewa chanjo ya corona, maafisa nchini Marekani wamesema.
Maafisa pia walikuwa wamesema baadhi ya wafanyakazi wa White House wanatarajiwa kupewa chanjo ya Pfizer/BioNTech wiki hii.
Chanjo hiyo inatoa ulinzi wa hadi asilimia 95 dhidi ya Covid-19 ana inaidhinishwa kuwa salama na wadhibiti wa dawa wa Marekani iliyopita Ijumaa.