
MBUNGE wa Buchosa, Mheshimiwa Eric Shigongo, ametembelea ujenzi wa zahanati ya Bulyaheke na kusisitiza watendaji pamoja na kamati ya ujenzi kuitisha mikutano ya wananchi na kuwasomea mapato na mamatumizi ili wananchi hao wafahamu namna ambavyo pesa yao zinavtumika.
Amesema kuwa wananchi wanatumia nguvu na rasilimali zao ili kufanikisha ujenzi wa maboma ya zahanati pamoja na madarasa hivyo hatacheka na mtendaji au mtu yeyote atakayethubutu kula fedha za wananchi katika Jimbo la Buchosa.
Aidha, ameongeza kuwa atafuatilia kwa karibu ukamilishwaji wa zahanati hiyo ili kuhakikisha fedha zinatumika vizuri na endapo kukitokea ubadhirifu wa aina yeyote hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika.
“Sitokuwa tayari kuona fedha za wananchi zinaliwa katika uongozi wangu, na niwaombe watendaji na watu wengine wanaohusika na ujenzi huu, waweke utaratibu wa mikutano na wananchi na kuwasomea mapato na matumizi kwani fedha hizi zinatoka kwenye mifuko yao.
“Na mimi kama mbunge wenu, nitashughulika na watu ambao watajaribu kula fedha za wananchi na hii ninawaambia watendaji na wananchi wote wa Jimbo la Buchosa,” amesma Shigongo.