Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, leo Desemba 16, 2020 amewaongoza mamia ya waombolezaji katika ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu 12 waliopata ajali mkoani Singida wakitokea Mwanza, tukio lililofanyika katika mtaa wa Nyerere B, kata ya Mabatini jijini humo.

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida baada ya gari aina ya Hiace waliyokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kuelekea Itigi kwenye sherehe za harusi kugongana uso kwa uso na lori la kubeba mafuta na kusababisha vifo vya watu 15 na majeruhi wawili.
