
BAADA ya kukamilisha usajili wa kiungo Mgan-da, Thaddeo Lwanga, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amependekeza usajili wa beki na mshambuliaji mmoja kwenye usajili huu wa dirisha dogo.
Juzi Jumanne, usajili wa dirisha dogo hapa nchini ulifunguliwa na unatarajiwa kudumu hadi Januari 15, mwakani.
Kwa mujibu wa Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, uongozi wa klabu hiyo tayari umepokea ripoti ya kocha huyo ambayo imetoa mapendekezo ya wachezaji watakaosajiliwa na kutolewa kwa mkopo.

Kaduguda alisema ripoti ya kocha huyo inahitaji wachezaji watatu pekee ambao ni beki wa kati, mshambuliaji na kiungo mkabaji ambaye tayari wamemchukua Lwanga.Aliongeza kuwa beki na mshambuliaji huyo tayari wamewapata ambao hivi sasa wapo kwenye taratibu za mwisho za kukamilisha usajili wao.“
Kama alivyosema mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi, Mo (Mohammed Dewji) kuwa usajili ni vita, hivyo ni lazima tufanye siri na kila kitu tutakiweka wazi baada ya taratibu za usajili kukamilika.“
Tumepokea ripoti ya kocha wetu Sven ambayo yenyewe imeagiza kuwa ni lazima tusajili wachezaji wawili ambao ni beki wa kati mwenye uwezo mkubwa atakayeisaidia timu katika michuano ya kimataifa.“
Pia ni lazima tumpate mshambuliaji mmoja mwenye uwezo zaidi au kama aliokuwa Bocco (John), Kagere (Meddie) na Mugalu (Chris) katika kuiimarisha safu yetu ya ushambuliaji,” alisema Kaduguda.
STORI NA WILBERT MOLAND | SPOTI XTRA