×

Kilichosemwa Mahakamani, Mabilioni ya Rugemalira, Seth – Video

 

UPANDE wa mashtaka umeeleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi inayowakabili mfanyabiashara, James Rugemarila, na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth na mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege wote kwa pamoja wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  upelelezi haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine.

 

Hakimu aliyesikiliza shauri hilo, Huruma Shaidi, ameahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa Desemba 30 mwaka huu.
Washtakiwa Seth na Rugemalira kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara kwa serikali Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

 

Mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, mwaka 2017. Pia  wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni.

Leave a Comment