×

Majaliwa Atoa Siku 7 Walionunua Magari ya Gharama Wajieleze

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa siku saba kuanzia jana (Alhamisi, Desemba 17, 2020) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, maofisa wanaochambua maombi ya ununuzi wa magari Ofisi ya Waziri Mkuu na wakurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halmashauri ya wilaya ya Chato, Msalala na Kahama wajieleze kwa sababu gani magari hayo yalinunuliwa kwa gharama kubwa.

 

Ametoa agizo hilo jana (Alhamisi, Desemba 17, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa umma, wabunge na madiwani katika jiji la Mwanza na manispaa za Ilemela na Nyamagana katika hoteli ya Malaika, jijini Mwanza. Amesema magari hayo ni mzigo kwa wananchi.

 

Amesema hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na haiwezekani viongozi hao watumie magari ya gharama kubwa badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na ametaka muongozo wa ununuzi wa magari, uliotolewa na serikali uzingatiwe.

 

Amesema matumizi ya fedha za umma lazima yasimamiwe ipasavyo na kwamba serikali haina mzaha na mtumishi yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha za umma, hivyo amewataka madiwani wakasimamie vizuri maeneo yao.

 

Leave a Comment