
WASANII watatu nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ na Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, usiku wa Desemba 20, 2020, wamefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kuibuka washindi kwenye tuzo za African Entertainment Awards, USA 2020 (AEAUSA) zilizofanyika huko New Jersey, Marekani.
Diamond Platinumz ametangazwa mshindi tuzo katika kipengele cha “Best Male Artist” (Msanii Bora wa Kiume) akiwashinda Eddy Kenzo, Wiz Kid , Shatta Wale, Stonebwoy, Davido, Burna Boy, Mohamed Abbas, Fally Ipupa na Jahllano ambao alikuwa akichuana nao kwenye kipengele hicho.
Malkia anayefanya vizuri, ‘Nandy’, ametangazwa mshindi wa tuzo katika kipengele cha “Best Female Artist” akiwashinda Zahara, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sho Madjozi, Sha Sha, Sheebah Karungi, Rema Namakula, Aya Nakamura na Kenza Morsli aliokuwa akichuana nao.
Msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB, Rayvanny, ametangazwa mshindi tuzo katika kipengele cha Best Male Artist – East/South and North Africa akiwashinda Elgrande Toto, The Ben, Diamond Platnumz, Alikiba Eddy Kenzo, Harmonize, Tewodros Kassahun AKA Teddy Afro, Jah Prayzah na Bruce Melodie aliokuwa akichuana nao.
Na Mtanzania mwingine aliiyeibuka na tuzo ni Dj Sinyorita ambaye ameshinda tuzo ya Best Dj
