×

Mwili wa Baba Jokate Ulivyoagwa Dar Leo

Jokate akifarijiwa na rafiki yake, Hamisa Mobeto.

Mwili wa Baba Mzazi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo, leo uliagwa na waombolezaji kwenye ibada iliyofanyika Kanisa la St. Peters Jijini Dar na hatimaye kusafirishwa kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma.

Katika ibada hiyo ndugu jamaa na marafiki walitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu na hatimaye msafara mazishi ulianza safari ya kuelekea Mbinga.

Wabunifu wa mitindo, Mustapha Hassanal (kushoto) na Martin Kadinda wakiwa kwenye ibada hiyo ya mazishi.
Mama Ndunguru ambaye ni mjane wa marehemu akimuaga mumewe.
Jokate akifarijiana na mtoto huyu wakati wa kuaga mwili wa marehemu.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mstaafu, Robert Manumba alivyopita kuaga.
Jokate alivyoongoza msafara baada ya mwili wa baba yake kuagwa.
Mwili ulivyoingizwa kwenye gari kwa ajili ya safari ya kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma.          HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave a Comment