×

JPM Amteua Sivangilwa Mwengesi Kamishina wa Maadili

RAIS John Magufuli, leo, Desemba 23, 2020, amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, akichukua nafasi ya Jaji Harold Nsekela ambaye alifariki dunia Desemba 6, 2020, jijini Dodoma.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi wa Jaji Mwangesi unaanza Desemba 23, 2020, na ataapishwa Desemba 24, 2020, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

Leave a Comment