
WAFANYABIASHARA wawili wa madini, Haji Hassan (52) na Jamas Hassan (55) wamehukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Miaka Mitatu Jela ama kulipa faini ya Sh. Milioni Moja kila mmoja kwa makosa ya kufanya biashara ya madini kinyume cha sheria.
Mahakama hiyo imewahukumu baada ya kutiwa hatia na mahakama hiyo kwa makosa ya kufanya biashara ya madini kinyume cha sheria.
Hukumu hiyo imetolewa leo Disemba 23, 2020, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya baada ya watuhumiwa hao kukiri makosa kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).
Watuhumiwa hao walishtakiwa mahakamani hapo kwa makosa ya kuhujumu uchumi Pamoja na kufanya biashara ya madini bila kuwa na kibali katika mtaa wa Lumumba na uhuru Kariakoo jijiji Dar es Salaam.
Awali watuhumiwa hao walimuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya kukiri makosa yao na kuomba kufunguliwa pazia la makubaliano yaani (Pree- Bargen) ambapo katika mazungumzo naye walitakiwa kulipa shilingi Milioni 40 kama fidia ya makosa hayo na tayari wamelipa.
Akitoa hukumu, Hakimu Isaya amesema kuwa madini hayo pia yatataifashwa na kwamba yatakuwa mali ya serikali ambapo mahakma hiyo imemkabidhi Wakili Mwandimizi wa serikali ili akayakabidhi kwenye mamlaka husika.
Watuhumiwa hao wamefanikiwa kulipa faini hiyo na wameachiwa huru.