×

Simba SC Wapania Kuimaliza FC Platinum

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, ameapa kula sahani moja na wapinzani wao FC Platinum watakaopambana nao leo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Simba itamenyana na FC Platinum katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa wapinzani wao.

 

Awali, Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya ligi hiyo baada ya kufanikiwa kuiondoa Plateau United ya nchini Nigeria kwa jumla ya bao 1-0 ugenini katika mchezo wa awali.Akizungumza na Championi Jumatano, Mkude alisema:-

“Mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wetu kujiandaa pia, kiukweli mwisho wa siku nimekuja kupambana kwa uwezo wangu wote, nina imani tutarudi na matokeo chanya nyumbani,” alisema Mkude.

 

Aidha kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalezamewataka Watanzania waendelee kuwasapoti kuelekea mchezo huo.

 

Ni nyota wawili wa kikosi cha Simba watakosekana ambao ni nahodha John Bocco na kipa namba moja Aishi Manula ambao waliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC

STORI: Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Leave a Comment