×

DJ Sbu Avunja Rekodi ya Dunia, Aipa Heshima +255 Global Radio

DJ na mjasiriamali kutoka Afrika Kusini, Sbusiso Leopo, maarufu kama DJ SBU ameendelea na kazi moja tu ya kuvunja rekodi ambapo awamu hii anaweka rekodi mpya duniani kwa kurusha matangazo mubashara kwa muda mrefu zaidi.

SBU ambaye anarusha matangazo hayo  kupitia redio yake iitwayo Home Grown Radio kwa muda wa wiki moja mfululizo pia ameungana na redio ya mtandaoni namba moja Tanzania ya +255 Global Radio.

Katika kuvunja rekodi hiyo Desemba 23 amerusha matangazo yake moja kwa moja kutoka studio za +255 Global Radio kwa muda wa saa moja.

SBU pia ametangaza tarehe ambayo video ya wimbo wake aliyomshirikisha msanii Alikiba itatoka na kuwaomba mashabiki wa muziki kumpa ushirikiano na kusaidia video hiyo kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya wiki moja.

“Ijumaa hii siku ya Krismas nitatoa video ya wimbo wangu niliyofanya na Alikiba, wimbo ambao unapatikana kwenye album yangu mpya, ninaaomba mnisaidie kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya wiki moja” alisema.

 

 

Leave a Comment