×

Sey Ataka Tuzo ya Ufungaji Afrika

MSHAMBULIAJI matata ndani ya kikosi cha Namungo FC, Steven Sey, ameibuka na kusema anatamani kuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Mshambuliaji huyo mpaka sasa anaongoza kwa mabao mengi kwenye michuano hiyo akiwa na mabao matatu katika michezo miwili ambapo yote timu yake ilicheza na timu kutoka Sudan, Al Rabita na Al Hilal.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sey alisema kuwa ni mipango yake kuja kuwa mfungaji bora kwenye michuano hiyo ya kimataifa. “Ni ndoto yangu kuwa mfungaji bora katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na nina imani nitafikia malengo yangu kwani najituma sana kuzidi kuwa bora.

 

Malengo yangu kama Mungu akipenda nitafunga kuanzia mabao 10 na kuendelea.”

Leave a Comment