
BAADA ya aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa ‘Basata’, Godfrey Mngereza kufariki dunia usiku wa kuamkia jana, chanzo cha kifo cha kiongozi huyo kimefahamika.
Akizungumza na Risasi Jumamosi jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa, Habbi Gunze alisema kuwa Mngereza alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Nimonia uliomlaza hospitali kwa takriban siku nne kabla ya kukutwa na umauti.“
Katibu alikuwa akisumbuliwa zaidi na ugonjwa wa Nimonia ambapo alilazwa katika Hospitali ya General iliyopo jijini Dodoma ya kumpumzisha ndugu yetu katika nyumba yake ya milele,”alisema kiongozi huyo.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abasi kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika ujumbe wa mwisho ambao aliupokea kutoka kwa marehemu kabla ya kufariki ambapo ulisomeka kama ifuatavyo:
“Nimelazwa General hapa Dom ila kila kitu kitaenda kwa siku zisizopungua nne hadi kufikwa na umauti, sisi kama baraza tunasikitika kutangaza msiba huu mzito katika tasnia ya sanaa kwa ujumla.“
Kikubwa kwa sasa ni kumuombea ndugu yetu ambaye nashindwa hata kumuelezea kutokana na alivyokuwa mtu makini na kwa sasa tunasubiri ratiba kutoka kwa familia na uongozi juu sawa kuhusu tamasha.
Napambana.”“Ni meseji ya mwisho niliyoipokea juzi Jumanne saa tano na dakika 2 usiku kutoka kwa kaka yangu Godfrey Mngereza, Katibu Mtendaji wa BASATA, leo hatunaye tena katika dunia hii. Ametutoka.Tumwombee sana, Mola ampe pumziko la amani la milele,”aliandika msemaji huyo wa SAAerikali.