
KITUO cha kutafiti uchumi na biashara kilicho na makao yake huko Uingereza CEBR kimesema kuwa Uchumi wa taifa la China utaupiku ule wa Marekani kufikia 2028, miaka mitano mapema ya ilivyokadiriwa ripoti.
Uwezo wa China kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona unatajwa kuimarisha ukuaji wake ikilinganishwa na Marekani na Ulaya katika kipindi cha miaka ijayo.
Wakati huohuo India inatarajiwa kuwa taifa la tatu lenye uchumi mkubwa duniani kufikia 2030, kituo hicho cha CBR hutoa matokeo ya utafiti wake kila mwaka tarehe 26 mwezi Disemba.
Pamoja na China kuwa nchi ya kwanza kuathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona, ilifanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo kupitia vitendo vyenye masharti makali ikimaanisha kwamba haikulazimika kusitisha kufunga baadhi ya maeneo na kufungua kama inavyofanyika barani Ulaya.

Kutokana na hilo ikilinganishwa na mataifa mengine yenye uchumi mkubwa , imefanikiwa kuzuia mfumuko wa kiuchumi mwaka 2020 na badala yake taifa hilo linatarajiwa kukua kwa asilimia 2 mwaka huu.
Uchumi wa Marekani umeathiriwa vibaya na virusi vya corona kulingana na takwimu. Zaidi ya watu 300,000 wamefariki nchini humo huku takriban watu milioni 18.5 wakiambukizwa .