×

Majaliwa Atua Ruangwa, Afanya Hili…

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa,  leo (Jumatatu, Desemba 28, 2020) amepokea vyumba 11 vya madarasa, ofisi mbili za walimu, samani na chumba maalumu cha wasichana vilivyojengwa na Benki ya TPB PLC katika shule ya msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa, Lindi kwa gharama ya shilingi milioni 164.902.

Amepokea mradi huo wa ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa alipotembelea shule hiyo akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa ambako ameupongeza uongozi wa benki hiyo.

Amewataka wazazi, walimu na wanafunzi wahakikishe majengo hayo yanatunzwa ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPB Bank PLC, Sabasaba Moshingi alisema utekelezaji wa mradi huo ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo wa kurejesha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya inayotekelezwa sehemu mbalimbali nchini.

Leave a Comment