
MUIMBAJI mkongwe wa nyimbo za Injili, rose Muhando amefunguka na kuanika mambo mazito aliyoyapitia kuhusu maisha yake huku akidai kuwa mambo mengine ameiachia Serikali kwani akiyasema yanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yake.
Rose amesema hayo leo wakati akizungumza na +255 Global Radio ndani ya kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6:00 mchana mpaka 12:00 jioni.
“Mini ukiniona niko kimya, sio kwamba sijui kuimba lakini ninafanya kazi yangu pale Mungu anaponiambia nifanye, siimbiimbi tu. Ninaimba kwa sababu. Mungu akisema nyamaza nina nyamaza, ukisema niimbe kufurahisha naimba tu lakini sio kusudi la Mungu.
“Nchi za wenetu wanatoa Tuzo kwa sababu zinakuwa zinawasaidia wasanii kupambana na kufanya vizuri zaidi, lakini kukosekana kwa Tuzo hapa kwetu kunatufanya tusisikike sana sababu zilikuwa zikitutangaza na ilikuwa inatusaidia kukufanya vizuri.
“Mungu amenipa ujasiri kama Simba, ningekuwa muimbaji mwingine ningeshaacha kuimba zamani. Nilipolazwa Nairobi Hospital nilitukanwa matusi sijawahi kuyasikia, lakini Mungu ndo mwenye kauli ya mwisho, sitishwi na watu ambao nao wanayo yaliyowashinda.
“Ukiona mtu anakutukana ujue uwezo wake wa kufikiria umefika mwisho, sababu matusi sio maisha na hayanisaidii, bora uje na kiboko unichape kuliko kunitukana, na mimi huwa sijibu vitu mitandaoni. Matusi yamekuwa kama shule kwangu.
“Mimi ni msiri sana, sijawahi kutumia madawa wala siyajui, nimepitia mambo magumu sana, ipo siku hivi karibuni jamii yote itajua ukweli uliofichwa, aliyenipeleka hospitali mpaka leo hajui nilikuwa naumwa nini, hajui kilichotokea nashukuru kutoka salama.
“Kuna mambo kwa ajili ya usalama wangu siwezi kuyaongea mimi, yanatakiwa yawe kwenye mikono tu ya Serikali, kuna watu wamehusika na hayo yaliyonitokea lakini ilianzaje… hapo ndo jamii itakuja kujua.
“Pamoja na matusi yote niliyotukana lakini Mungu amekuja akanipa Tuzo ambayo nimeshinda hivi karibuni nchini Burundi…. (Edge Gospel Music Award Burundi, kipengele cha Muimbaji Bora wa Kike Afrika Mashariki).
“Mwaka 1990 nilikuwa mgonjwa sana, tulihangaika na wazazi wangu ikashindikana, siku moja saa 9 usiku niliona mwana wa duara mfano wa nguzo ukatokeza mkono ukanigusa kichwani, sauti ikasikika “mimi ni Yesu nimekuponya amka ukanitumikie, wazazi wangu waliona na macho.
“Wazazi wangu walishuhudia kwa macho yao niliyofanyiwa na Mungu ili baadae isije ikawa labda kuna kitu. Kuanzia hapo nikabadili dini kutoka Uislam nilikuwa naitwa Shadya, nikabatizwa na kuitwa Rose, nikaanza kuimba na kufundisha kwaya, Mungu amenitunza.
“Watoto wangu hawana baba, yupo lakini kama hayupo, hiyo ni stori ndefu sana… mimi nimeishi maisha ya mtaani, nikaja kuchukuliwa na Bishop Maboya akanifundisha neno la Mungu baadaye akanishauri nikarudi kwa wazazi nikiwa na watoto wangu na wazazi wakanipokea.
“Watoto wangu hawana baba, yupo lakini kama hayupo, hiyo ni stori ndefu sana… mimi nimeishi maisha ya mtaani, nikaja kuchukuliwa na Bishop Maboya akanifundisha neno la Mungu baadaye akanishauri nikarudi kwa wazazi nikiwa na watoto wangu na wazazi wakanipokea.
“Watu huwa wanachanganya, Msama hakuwa meneja wangu, alikuwa mtu wa promosheni kwangu, kuandaa matamasha na tulifanya kazi kama familia lakini sababu alihusika na mambo yangu mengi hivyo watu wengi walimuita kama meneja wangu.
“Albamu ya kwanza nilirekodi kwa Master J, sikujua chochote, nilirekodi albamu nikaiweka tu, wao ndo walionipeleka kwa Wahindi (GMC) nikiwa na ndala zangu, wakasimamia nikasaini nikaanza kulipwa, hawakuchukua hata mia, wangekua wezi wangekuwa wa kwanza kuniibia,” amesema Rose Muhando.