×

Amber lulu Amtolea Uvivu Uchebe

BAADA ya mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe kuposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa na msanii Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ na kusindikiza na maneno yaliyoashilia kuwa mrembo huyo ana ujauzito wake, hatimaye Amber ameibuka na kumtolea uvivu kwa kumwambia kuwa amkome.

Akizungumza na Risasi Vibes, mrembo huyo amesema aliamua kuandika mtandaoni kuwa Uchebe amkome kwa sababu yeye ndio kaanza kufanya hivyo lakini pia ilikuwa ni kutaka kujisafisha kwa mambo ya kijinga anayoyaongea Uchebe juu yake.

 

“Niliamua kumjibu palepale kwenye posti yake bila kukwepa kwa sababu Uchebe hajitambui, namheshimu sana Shilole ni kama dada yangu sasa kama anataka kiki ni kwa hao wanawake wengine sio kwangu, nataka aniheshimu kama dada yake,” alisema Amber

Leave a Comment