
MWILI wa aliyekuwa katibu mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, umeagwa kwa mara ya mwisho jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Karimjee.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria katika hafla hiyo akiwemo Waziri wa sanaa, Innocent Bashungwa, Naibu wake, Abdallah Ulega, katibu mkuu wake, Dkt Hassan Abbas, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Aboubakary Kunenge na wengine wengi.