×

Egla Mamoto; Kada wa CCM Azikwa Dodoma

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Egla Mamoto, amezikwa jana Jumanne, Desemba 29, 2020 katika Kijiji cha Mpwayungu, wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Enzi za uhai wake Egla aliwahi kuwa Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Vijana wa (CCM).

Mamoto ambaye katika uchaguzi wa mwaka huu aligombea ubunge kupitia kundi la wazazi, amefariki katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia Jumapili Desemba 27, 2020.  Ameacha mume na mtoto mmoja.

Katika uhai wake alikaimu kama Katibu wa Uhamasishaji Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja 2015/16 ambapo katika kipindi hicho alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa UVCCM.

 

 

 

 

 

 

Leave a Comment