
RAIS John Magufuli ameeleza namna ambavyo Mungu alimwepusha na kifo wakati akitoka kuposa baada ya kusita kupanda boti ya Busisi-Kigongo akihofia usalama wake lakini baada ya boti hiyo kuanza safari ilizama na kuua watu 11.
Magufuli amesema hayo wakati akiwa jijini Mwanza akikagua mradi wa ujenzi wa Daraja la Magufuli (Daraja la Kigongo- Busisi) ambalo linapita juu ya Ziwa Victoria.