
RAIS John Magufuli leo tarehe 31 Desemba, 2020, amewasilisha fomu zake za maadili katika ofisi ya makao makuu ya Sekratarieti ya Maadili ya viongozi Jijini Dodoma.
Katibu wa Rais, Ngusa Samike, amekabidhi fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi.
Leo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maadili kwa viongozi wote kwa mujibu wa Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
