×

Wananchi Wamshukuru Shigongo kwa Hili… – Video

 

WANANCHI wa Kijiji cha Sukuma, Halmashauri ya Buchosa, wameeleza furaha yao baada ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa kwa pamoja wakishirikiana na ofisi ya mbunge na halmashauri hiyo katika shule mpya ya Sekondari ya Sukuma.

 

Wananchi hao wameeleza kuwa kukamilika kwa shule hiyo kutapunguza adha walizokuwa wanazipata wanafunzi kwa kuacha masomo kutokana na umbali na wengine kupata ujauzito.

 

 

Hayo yamejiri wakati Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, alipotembelea kukagua shule hiyo ambapo amewahimiza wanachi wa Sukuma na jimbo hilo kwa jumla kuendelea kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

 

Shigongo amewataka wazazi kupeleka watoto wao shuleni  pindi tu shule zitakapofunguliwa ili wakapate elimu kwani ndiyo silaha kubwa ya mafanikio ya mtoto na taifa kwa jumla.

TAZAMA VIDEO KAMILI

Leave a Comment