×

Wawili Waula Safari ya Kutalii Ngorongoro

Afisa Msimamizi wa Fedha wa GSM, Raphael Mwakasege akizichanganya kuponi kabla ya kuchagua moja ya ushindi kushoto Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga akihakiki mambo yanavyokwenda.

WATANZANIA wawili wameula kwa kujishindia safari ya kwenda kutembelea hifadhi ya Ngorongoro kwenye Promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na maduka ya GSM kwa wateja waliokuwa wakifanya manunuzi kwenye maduka hayo.

Washindi hao wamepatikana katika droo ya tatu na ya nne zilizochezeshwa kwenye duka la GSM Msasani jijini Dar ambayo iliwakirisha maduka yao mengine.

Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga alisoma jina la mmoja wa washindi wa safari ya Ngorongoro.

Katika promosheni hiyo washindi wengine wawili walipata vocha ya manunuzi dukani hapo ya laki tano kila mmoja na wawili wa mwisho waliambulia vocha ya manunuzi laki mbili na nusu kila mmoja.

Akizungumza katika promosheni hiyo Afisa Masoko wa GSM, Fatma Farah amewashukuru wateja hao kwa kuwaunga mkono kwenye maduka yao na kuwakaribisha tena.

Afisa Masoko wa GSM, Fatma Farah, akimpigia simu mshindi wa safari ya Ngorongoro kumpa habari za ushindi wake.

Fatma aliwataja wateja waliojishindia safari hiyo kuwa ni Loreen Raymond na Mathew Kauranda ambapo Florence Gondwe na Zain Lookmanji wakijishindia vocha ya manunuzi ya laki tano kila mmoja na mwisho Aliakber Nuri na Michael Nachipyang wakiondoka na vocha ya manunuzi ya shilingi laki mbili na nusu kila mmoja.

Droo hiyo ilichezeshwa mbele ya wanahabari na kusimamiwa na msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga.

Leave a Comment