
ESMA Khan, dada wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ naye ni maarufu. Umaarufu wake ulitokana na jina la kaka yake lakini hivi sasa naye anajibeba mwenyewe.
Hivi karibuni ‘alitrendi’ kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa yake iliyodumu miezi minne tu na kurudi kwa baba mtoto wake, Petitman.
AMANI lilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya ana kwa ana kama ifuatavyo:
Amani: Habari Esma, mzima…
Esma: Salama, leta habari za Global maana hamna dogo nyie.
Amani: Hapana tupo tu, tunataka mpya kutoka kwako.
Esma: Haya nipo tayari, najua maswali yenu.
Amani: Umekuwa kimya sana baada ya harusi, kwa nini maana hata kwenye mitandao umejiondoa kabisa, mume alitaka hivyo?

Esma: Hapana, niliamua mwenyewe kujituliza akili yangu yaani hata kwenye mitandao sikuonekana kabisa, niliamua kwanza niwaumize kichwa walimwengu.
Amani: Watu walidhani kuwa mume kakuzuia mitandaoni?Esma: Hawezi kunizui kwa sababu alinikuta hivyo isipokuwa niliamua kuwa hivyo mwenyewe tu.
Amani: Vipi kuhusu biashara yako maana hata watu walikuwa wakienda pale hawakuoni kabisa.
Esma: Nilipumzika nyumbani kwa muda wa miezi minne, nikaamua kuwaachia wasichana wangu dukani.Amani: Unajua watu wengi wanajua wewe ni boss lady kwa sababu ya kaka, hii unaiongeleaje?
Esma: Pesa za Nasibu, haziwezi kuwa zangu, atayekula hela labda mama yake na hilo liko wazi na hata kama kunisaidia basi itakuja tu…
Amani: Kwenye mitandao zilizagaa picha ukiwa hoi unaumwa, nini zaidi kilikuwa kikikusumbua?

Esma: Nilikuwa tu sina damu lakini sikuwa na shida yoyote ile.
Amani: Mbona kulikuwa na madai kuhusiana na kutoa ujauzito wa mumeo na mpaka akaweka kwenye mtandao wake wa Instagram mshumaa?
Esma: Itakuwa labda alikumbuka vitu vingine lakini mimi sijawahi kutoa mimba kabisa.
Amani: Watu wengi walidhani kuwa ulipokuwa ukisema mambo ya Mama Melo labda ni utani kumbe kweli ni mke mwenzako, ilikuwaje sasa?
Esma: Ni kweli kwani hata nilipoolewa si nilikuwa najua ni mke wa tatu.Amani: Sasa vipi kuhusu madai ya kuachana au bado uko kwenye ndoa yako?Esma: Hapana niko single.Amani: Lakini ndoa yako itakuwa imevunja rekodi, miezi mitatu imevunjika?
Esma: Ukiwa mkweli na uhuru utaishi maisha mazuri, wataofi kiria nimevunja rekodi haya.Amani: Kuna madai kuwa umerudiana na mtalaka wako Petitman, vipi kuhusu hizo habari?
Esma: Ila watu wana vituko sana wanashindwa kutambua kuwa yule ni baba mtoto wangu, walitaka hata nisisalimiane naye.Amani: Kwenye msiba wa mama yake Petitman, mlionekana karibia familia nzima mmeenda sasa kwa upande wa mumeo wanasema hilo?
Esma: Upande upi tena, na hata kama tumeenda tuna haki kabisa, kwa sababu ni bibi wa mwanangu na alikuwa rafi ki yangu sana.
Amani: Kwenye msiba Petit hakuweza kufi cha hisia maana kila mara alikuwa anakufuata, hii ikoje?Esma: Umesahau kuwa penzi la kweli halifi , linakuwepo tu hata kama mtu anaoa au anaolewa.
Amani: Hivi karibuni alikuja Zari pamoja na watoto lakini sikukuona umeenda au kupiga naye picha hata moja japo ulionekana kufurahi sana ujio wake, kwa nini?
Esma: Ni kwa sababu na mimi nilikuwa kwenye harakati zangu lakini tuliwasiliana.Amani: Alivyokuja Zari, hukutamani aendelee kukaa moja kwa moja Kama wifi ?
Esma: Zari ni mama wa watoto wetu na pia kuhusu wifi hilo ni jukumu la yeye Diamond mweyewe.Amani: Uliweka wazi kuwa gari ulilozawadiwa halikuwa la kweli, nini kilitokea sasa?
Esma: Sijajua lakini kweli halikuwa langu maana lilirudi lilipotoka na ninachoshukuru nina langu ndio hivyo.
Amani: Kwenye mtandao niliona ulimuweka wazi baba wa mtoto wako wa kwanza, ulifi kiria nini?
Esma: Ni kwa sababu ni baba yake na niliamua kuweka wazi na hata mwanangu ajisikie vizuri.
Amani: Kwa hiyo bado unakaa kwenye nyumba aliyokupangia mumeo.Esma: ( kicheko) Hilo siwezi kulijibu kwa sasa.Amani: Haya nakushukuru sana.Esma: Shukurani.
Makala: IMELDA MTEMA