×

Iran Kurutubisha Madini Yake ya Uranium kwa Asilimia 20

Iran inapanga kuanza tena kurutubisha madini yake ya uranium, kwa asilimia 20, hayo ni kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA), hatua ambayo hadi kufikia sasa itakuwa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kimataifa ya nyuklia.

 

Hiyo inamaanisha kwamba Iran itakuwa na upungufu wa asilimia 80 ya kiwango kinachohitajika kutengeneza bomu la nyuklia.

 

Lakini kulingana na makubaliano ya mwaka 2015, Iran ilihitajika kuimarisha madini yake ya Uraniaum kwa kiwango cha chini ya asilimia 4.

 

Iran ilianza kukiuka makubaliano hayo baada ya Rais Trump kuindoa Marekani kwenye makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa na kuiwekea tena nchi hiyo vikwazo. ambavyo vimeyumba pakubwa uchumi wa nchi hiyo.

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA), limesema Iran ilikuwa imeifahamisha mpango wake wa kurutubisha madini yake ya uraniaum hadi asilimia 20 katika mtambo wake ambao umejengwa ndani ya mlima lakini shirika hilo limeongeza: “Barua ya Iran haikusema shughuli hizo zitataanza lini.”

 

Iran ilikiuka kiwango ambacho kilikuwa kimewekwa kwa uimarishaji wa madini yake cha asilimia 3.67 kulingana na makubaliano ya nyuklia yam waka 2019 lakini Iran iliamua kuendeleza kiwango hicho kwa hadi asilimia 4.5 tangu wakati huo.

 

Leave a Comment