×

Majeruhi Ajali ya Treni Waruhusiwa Kutoka Hospitali


MAJERUHI  54 wa ajali ya treni iliyotokea Dodoma waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo, wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya hali zao kuimarika huku wengine 12 wakiendelea na matibabu.

Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt Ernest Ibenzi, na kubainisha kwamba majeruhi 12 wanaoendelea na matibabu, hali zao zinaendelea vizuri na baadhi yao wanaweza kuruhusiwa wakati wowote.

 

Treni ya abiria kutoka Dar es salaam ilianguka juzi jioni wakati inakaribia kituo cha Bahi kutoka stesheni ya Kigwe na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 66.

Leave a Comment